Wanawake ambao ni wa Freemason na itikadi zao


Wanawake wa Freemason wamekuwa wakikongamana kwa zaidi ya miaka 100 sasa - wakifanya matambiko na sherehe sawa na wenzao wa kiume.
Lakini si watu wengi wanaofahamu kuwepo kwa kundi hili. Sasa tunaweza kukufahamisha zaidi kuhusu shughuli za Freemason hawa wa kike baada ya kipindi cha redio cha Victoria Derbyshire cha BBC kuruhusiwa kuzungumza nao.
"Freemason ni nani?" anauliza mmoja wa viongozi wao ambao huitwa master (gunge) katika Kongamano Tukufu la Jumuiya ya Freemason wa Kale.
"Ni mfumo wa kipekee wa maadili ambao umezingirwa na istiari na ishara zenye maana," anajibu Dialazaza Nkela.
Nkela anashiriki katika sherehe ya kipekee ya kumfikisha ngazi ambayo hufahamika kama "shahada ya pili".
Ni sherehe ya kusherehekea kupanda hadhi kwake katika kundi lake.
Kufikia kwake "shahada ya kwanza" kuliadhimishwa kwa kuingizwa kwake katika kundi hilo, shughuli ambayo ilihusisha yeye kuweka wazi "mkono wake wa kulia, ziwa lake la kulia na goti la kulia" kitanzi kikiwa kimewekwa kwenye shingo lake.
Kila sehemu ya tambiko hilo, hudaiwa kuwa na maana yake - ingawa hatukufahamishwa zaidi.
Dialazaza Nkela being questioned by the grand master
Image captionDialazaza aliulizwa maswali kuhusu ni kwa nini ufreemason ni muhimu kwake
"Shahada ya tatu" hudaiwa kuwa "pale unapokumbana na kifo ili kuzaliwa upya" na huwakilishwa na "mwisho wa uhai mmoja na kuanza kwa maisha mengine".
Maana ya hili pia, wanaweka siri.
Lakini ufichuzi huu wenyewe ni kidokezo kuhusu shughuli na imani za kundi hili lenye usiri mkuu.
Watu wengi hata huwa hawafahamu kwamba kuna mafreemason wa kike.
Freemason wa kiume - ambao walianza rasmi mikutano yao zaidi ya miaka 300 - wamekuwa wakiangaziwa zaidi.
Kwa sasa huongozwa na mwanamfalme mtawala wa Kent.
Lakini ukijumlisha makundi mawili yaliyopo ya freemason wa kike - Honourable Fraternity of Ancient Freemasons na Order of Women Freemasons, ambayo yaligawanyika mapema karne ya 20 - kuna karibu mafreemason wa kike 5,000.
Honourable Fraternity of Ancient Freemasons
Image captionWanachama wa kundi la Kongamano Tukufu la Jumuiya ya Freemason wa Kale hukutana katika hekalu kama hili
Wanachama wa Order of Women Freemasons hukutana mara kwa mara katika mahekalu au nyumba kote nchini Uingereza.
Wakati wa sherehe zao, wanawake huvalia gauni ndefu za rangi nyeupe pamoja na mapambo shingoni kuashiria cheo cha kila mwanachama.
Ibada zao huanza kwa msafara kwenye njia kuu ya kuelekea kwenye madhabahu ndani ya hekalu.
Wanachama wa kundi hilo huinama wanapofika pale mbele, ambapo huwa ameketi mkuu wao ambaye hufahamika kama grand master (gunge mkuu).
Grand master (Gunge mkuu) wa sasa ni Zuzanka Penn ambaye huketi katika kiti kikuu ambacho hufanana na kiti cha enzi.
Huwa kuna maombi wakati wa ibada zao, na wakati mwingine unaweza kuhisi kana kwamba hilo ni kundi la kidini, ingawa Bi Penn anasisitiza wkamba hilo si kundi la kidini.
"Ili uwe wa Freemason, lazima uwe umeamini katika kiumbe (au roho) mkuu," anasema, lakini unaweza kuwa katika "imani (dini) yoyote ile".
"Huwa tuna watu ambao wana imani sana kidini, na wengine ambao hawafuati sana dini - lakini ni watu wa asili mbalimbali, au imani mbalimbali," anasema.
Order of Women FreemasonsHaki miliki ya pichaORDER OF WOMEN FREEMASONS
Image captionWamasoni huvalia mapambo kuashiria vyeo vyao
Wengi wa wanawake wamasoni huwa wana miaka 50 na kwenda juu - jambo ambalo wanataka sana kubadilisha.
Kwa sasa, wanawatafuta wanawake vijana, wakiwemo wale waliojiunga na vyuo karibuni, wawe wanachama.
Mtaalamu wa macho Roshni Patel anafanyiwa sherehe ya kumfanya kuwa wa ngazi ya Mastre katika kundi hilo.
Alijiunga na Freemason miaka saba iliyopita.
Hatukuruhusiwa kuhudhuria sherehe hiyo, lakini tunafahamu kwamba alipewa "heshima" ya kuketi kwenye kiti kile kinachofanana na kiti cha enzi.
"Shughuli yote ya kuwekwa kwenye kiti hicho, ilikuwa ya kuteka hisia sana," anasema, akiondoka.
Roshni Patel
Image captionRoshni amekuwa freemason gunge
"Hasa kwa wanachama wote wa nyumba yetu, ambao wananidhamini sana."
Alipoulizwa kuhusu kuwa Freemason wa ngazi ya master (gunge), aliongeza: "Bado nina mshangao," huku akijaribu kukubali uhalisia wa ufanisi wake.
Lakini kikwazo kikuu zaidi pengine kwa wale wanaotaka kujiunga na kundi hilo huwa ni sifa zake za usiri mkuu pamoja na kuhusishwa kwake na ufisadi.

1 comment:

  1. MALI,UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI MPAKA MASAA 72(SIKU 3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.